great chiefs in chagga tribe

in chagga language they are known as mangi
Those famous chiefs includes
mangi rongoma of kilema
mangi horombo of keni
mangi rengwa of machame
mangi mashina of mamba
mangi mosha of kirua
mangi marealle of marangu
mangi sina of kibosho
mangi rindi of moshi
mangi meli of moshi
mangi warsingi of uru
mangi ndeseruo of machame
mangi shangali of machame
mangi lokila of kibosho
mangi kikare of kirua
mangi kombo of kilema
mangi masaki of kilema

Saturday, April 16, 2011

uchaguzi katika jimbo la vunjo

uchaguzi huu ulimalizika kwa kushuhudia jimbo kuu la upinzani kwa mara nyingine tena katika historia likirudi kwenye kambi ya upinzani baada ya miaka mitano ya kuongozwa na ccm chini ya mheshimiwa aloyce bent kimaro maarufu kwa jina la 'nakara' ambaye alisifika katika bunge la tisa kama miongoni mwa wabunge walioichachafya zaidi serikali na kambi ya mafisadi kwa ujumla
mchuano ulikuwa kati ya wafuatao
1.augustino lyatonga mrema tlp
2.john mrema chadema
3.chrispin meela ccm
baada ya mchuano na kampeni kali kabisa kushuhudiwa huku zikichagizwa na wanafunzi pamoja na vijana chama tawala kiliangushwa vibaya baada ya mrema kufanikiwa kupata ushindi wa kishindo(tlp)
hivyo jimbo la vunjo limeingia katika historia ya majimbo yaliyoongozwa na vyama vitatu kwa nyakati tofauti
kama ifuatavyo
ccm,nccr,tlp
2.ubungo
ccm,nccr,chadema
3.iringa mjini
ccm,nccr,chadema
4.mbeya mjini
ccm,nccr,chadema
5.hai
ccm,nccr,chadema

uchaguzi katika jimbo la vunjo

uchaguzi huu ulimalizika kwa kushuhudia jimbo kuu la upinzani kwa mara nyingine tena katika historia likirudi kwenye kambi ya upinzani baada ya miaka mitano ya kuongozwa na ccm chini ya mheshimiwa aloyce bent kimaro maarufu kwa jina la 'nakara' ambaye alisifika katika bunge la tisa kama miongoni mwa wabunge walioichachafya zaidi serikali na kambi ya mafisadi kwa ujumla
mchuano ulikuwa kati ya wafuatao
1.augustino lyatonga mrema tlp
2.john mrema chadema
3.chrispin meela ccm
baada ya mchuano na kampeni kali kabisa kushuhudiwa huku zikichagizwa na wanafunzi pamoja na vijana chama tawala kiliangushwa vibaya baada ya mrema kufanikiwa kupata ushindi wa kishindo(tlp)
hivyo jimbo la vunjo limeingia katika historia ya majimbo yaliyoongozwa na vyama vitatu kwa nyakati tofauti
kama ifuatavyo
ccm,nccr,tlp
2.ubungo
ccm,nccr,chadema
3.iringa mjini
ccm,nccr,chadema
4.mbeya mjini
ccm,nccr,chadema
5.hai
ccm,nccr,chadema

marangu

watu wa kwanza waliokuja kukaa marangu ni wataita.
baada ya kufika hao wengine wakaja kutoka ugweno,kahe na arusha chini.
wengi katika hao walikaa kilema na mamba,
lakini wachache walifata mto kimo na kuja kukaa marangu
wote walikuwa hawana mali, na wote walikaa hivi hivi mpaka wale waliokaa mshiri walijichagulia  mkuu wao jina lake kilaweso.
labda kilaweso alikuwa mkuu wa wachagga,na  kwa hivi tutaona jinsi alivyopata ukuu wake,na jinsi ukuu wake ulivyokwisha.
imehadithiwa ya kuwa siku moja kilaweso alimwua mtu mmoja aliyeua mtu mwingine mbele ya macho yake ,na kwa kuwa watu wote walikuwa wamwechoka kabisa na mauaji na fujofujo, walipendezwa na tendo lake,wakamfanya mwamuzi wao,wakampa ruhusa ya kuwaadhibu wahalifu wote katika nchi, na malipo yake walimwahidia kumjengea nyumba na  kumlimia mashamba yake,
huu ndio mwanzo wa desturi waliyonayo wachagga ya kuwalimia na kuwajengea nyumba wakuu wao,
kilaweso alikuwa mwenye nguvu nyingi tena shujaa kama simba na kabla hazijapita siku nyingi aliiweka nchi ikae kwa taratibu

Thursday, July 29, 2010

Horombo

Hapo mwanzo wakuu wa mamba waliwashinda sana watu wa rombo kwa kuwa hapakuwa na mkuu yeyote katika nchi ya Rombo wakati huo,ila kulikuwa na watu wachache wachache mno walioongozwa na wakubwa wao,kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine za kilimanjaro kabla ya kusimamishwa wakuu. Katika nchi ya useri tu kulikuwa na mkuu,lakini useri haikuwa sehemu ya milki ya mamba,mtu mmoja jina lake moosinyi wa ukoo wa kumba alikuja na wafuasi wake wakakaa keni,na kijukuu chake jina lake ukongi alipigana na marawite wa mamba kwa muda,ingawa alishindwa, hata hivi alifanywa mkubwa wa nchi ya chimbili chini ya marawite.chimbili ni nchi iliyokati ya mriti na mkuu.urio mwanae ukongi alimuari mafuluke,pia akashindwa baada ya vita vikali vya siku nyingi.katika vita hivi nchi iliachwa ukiwa wala haikuwa na ng'ombe,lakini mafuluke aliweka ng'ombe wake wengine kwa watu,na kwa miaka kadhaa walikaa kwa amani chini yake
urio alikuwa na wana wawili,mkubwa alikuwa Msangaro na mdogo aliitwa Horombo.
Msangaro alikuwa kijana mpole lakini horombo alikuwa mkali wala hawezi kutulia,akamwudhi sana baba yake kwa kuwaua ng'ombe waliowekwa kwao na watu wa mamba na kuila nyama yake,alikuwa na nguvu nyingi sana,tena mrefu kuliko watu wote wa nchi,hivyo hakuna aliyethubutu kumchokoza,katika ujana wake alijipatia sifa nyingi kwa sababu alimwua tembo peke yake,na watu wa waalenyi walipokuja kuchukua nyama ya tembo,aliwanyang'anya ng'ombe wao wote na kuwachinja kuwafanyia karamu watu,matendo aliyoyafanya yaliwaogofya sana watu wa keni mpaka walimwomba awe mkuu wao,maana waliona hakuna njia ila hii ya kupata amani katika nchi.
Lakini watu wa nchi zilizo jirani,yaani mriti,mengeve,chimbili, na mkuu hawakumkubali horombo,na kwa hivi alifanya vita nao akawanyanga'nya ng'ombe wengi sana.lakini ng'ombe wale aliowachukua kwa kweli walikuwa ng'ombe za watu wa mamba,

Rombo

Kadiri ilivyojulikana,habari za zamani
rombo ni habari za jamaa nyingine ambazo hapana moja iliyokuwa ya maana sana.hapakuwa na mkuu katika nchi ya rombo mpaka wakati wa HOROMBO,na hata hivyo haikudumu sana baada ya kufa horombo isipokuwa katika useri.
Sababu ya tofauti kubwa ya warombo na wachaga wengine si vigumu kuieleza,nchi ya rombo ni nzuri kwa mifugo ya ng'ombe,lakini sehemu nyingine ya kilimanjaro inayokaa watu ni nchi ya kilimo hasa.wachaga hasa walikuwa walimaji,lakini warombo walipenda kufuga ng'ombe
na sababu ya tofauti ni hizi
1.kwa desturi watu wafugao ng'ombe hawashirikiani sana pamoja
wanapenda zaidi kukaa kila jamaa peke yake,hivyo warombo walishika desturi zao za zamani walizozipata kutoka ukamba ambako hapakuwa na wakuu wa kutawala
2.wale waliokuwa walimaji walitamani sana kupata ng'ombe ,hivyo walikuwa tayari kujiweka chini ya mkuu awezaye kupigana na jirani na kukamata ng'ombe zao hivyo kuwatajirisha kwa mifugo
3.mifereji ya maji kwa walimaji haikuwezwa kutengenezwa na kuangaliwa bila watu kushirikiana pamoja chini ya wakuu waliojulikana au kuchaguliwa. Lakini nchi ya Rombo ni kavu,wala haina vijito vilivyo lazima kutumika katika mashamba.basi hapo warombo walikuwa hawana haja ya kujiweka chini ya watawala,ndiyo sababu wakuu hawakuwekwa katika nchi yao.