great chiefs in chagga tribe

in chagga language they are known as mangi
Those famous chiefs includes
mangi rongoma of kilema
mangi horombo of keni
mangi rengwa of machame
mangi mashina of mamba
mangi mosha of kirua
mangi marealle of marangu
mangi sina of kibosho
mangi rindi of moshi
mangi meli of moshi
mangi warsingi of uru
mangi ndeseruo of machame
mangi shangali of machame
mangi lokila of kibosho
mangi kikare of kirua
mangi kombo of kilema
mangi masaki of kilema

Thursday, July 29, 2010

Rombo

Kadiri ilivyojulikana,habari za zamani
rombo ni habari za jamaa nyingine ambazo hapana moja iliyokuwa ya maana sana.hapakuwa na mkuu katika nchi ya rombo mpaka wakati wa HOROMBO,na hata hivyo haikudumu sana baada ya kufa horombo isipokuwa katika useri.
Sababu ya tofauti kubwa ya warombo na wachaga wengine si vigumu kuieleza,nchi ya rombo ni nzuri kwa mifugo ya ng'ombe,lakini sehemu nyingine ya kilimanjaro inayokaa watu ni nchi ya kilimo hasa.wachaga hasa walikuwa walimaji,lakini warombo walipenda kufuga ng'ombe
na sababu ya tofauti ni hizi
1.kwa desturi watu wafugao ng'ombe hawashirikiani sana pamoja
wanapenda zaidi kukaa kila jamaa peke yake,hivyo warombo walishika desturi zao za zamani walizozipata kutoka ukamba ambako hapakuwa na wakuu wa kutawala
2.wale waliokuwa walimaji walitamani sana kupata ng'ombe ,hivyo walikuwa tayari kujiweka chini ya mkuu awezaye kupigana na jirani na kukamata ng'ombe zao hivyo kuwatajirisha kwa mifugo
3.mifereji ya maji kwa walimaji haikuwezwa kutengenezwa na kuangaliwa bila watu kushirikiana pamoja chini ya wakuu waliojulikana au kuchaguliwa. Lakini nchi ya Rombo ni kavu,wala haina vijito vilivyo lazima kutumika katika mashamba.basi hapo warombo walikuwa hawana haja ya kujiweka chini ya watawala,ndiyo sababu wakuu hawakuwekwa katika nchi yao.

No comments:

Post a Comment