great chiefs in chagga tribe

in chagga language they are known as mangi
Those famous chiefs includes
mangi rongoma of kilema
mangi horombo of keni
mangi rengwa of machame
mangi mashina of mamba
mangi mosha of kirua
mangi marealle of marangu
mangi sina of kibosho
mangi rindi of moshi
mangi meli of moshi
mangi warsingi of uru
mangi ndeseruo of machame
mangi shangali of machame
mangi lokila of kibosho
mangi kikare of kirua
mangi kombo of kilema
mangi masaki of kilema

Thursday, July 29, 2010

Rongoma

katika habari za kilema tulifika mpaka wakati wa kombo alipourithi utawala toka kwa Nyange.katika utawala wake,kilema iliingiliwa na Ngaramite mkuu wa marangu aliyesaidiwa na watu wa chimbili na wengine wa ugweno.Kombo alikimbia pamoja na watu wake wote mpaka Kirua alipotawala MOSHA.Basi ikatokea ya kuwa Mosha alimtamani mkewe Kombo akajaribu kumshawishi ampe sumu mumewe na mwanawe RONGOMA pia.lakini yule mwanamke alikimbia akarudi kilema,na Kombo na watu wote walimfuata.mara alipopata habari hii,ngaramite aliingia tena kilema pamoja na rafiki zake wagweno.kombo alitaka kukimbia tena,lakini mke wake alijipatia silaha akawaongoza watu wa kilema kupambana na adui,na hapo Kombo akaona aibu,na yeye mwenyewe akaja akawaongoza.nao watu wa kilema walijipa moyo kwa kuona ushujaa wa yule mwanamke,wakapigana kwa nguvu nyingi sana wakawashinda adui zao.
Baada ya hayo Kombo alinuia kumpiga Mosha kwa kufanya lile tendo ovu wakati alipokuwa mgeni wake.akampeleka mwanawe Rongoma utaita ili apate msaada lakini alikawia sana,na huku nyuma yeye mwenyewe alipata msaada kutoka ugweno akawashinda watu wa Mosha,akawaweka chini yake,baada ya muda kupita Rongoma alirudi kutoka utaita akileta watu wa kupigana pamoja nae,na kwa kuwa nchi ya kirua ilikwisha wekwa chini ya baba yake,walifanya vita na marangu iliyotawaliwa na masanjuo,wakateka sehemu ya nchi ile.
Baada ya miaka michache kupita kombo alijiuzulu na mwanawe RONGOMA Akaushika utawala.wakati huo huo kilewo aliyekuwa mtawala wa marangu akafa pia,mara ile Rongoma alipeleka tarishi kuwakaribisha wanawe kilewo waje kukaa nae ili apate kuwatunza,maana kwa kuwa ni mzao wa mremi alifanya kama anataka kuwa kaka yao,silawe na ishosho wana wawili wa kilewo walikwenda kilema wakapokewa vizuri,lakini walipotaka kurudi kwao,Rongoma aliwafanya wafungwa,kisha aliingia marangu na kujitangaza mkuu kwa haki,kwa kuwa ni mkubwa wa ukoo, uliotoka wakuu wa nchi zote mbili.

No comments:

Post a Comment