Hapo mwanzo wakuu wa mamba waliwashinda sana watu wa rombo kwa kuwa hapakuwa na mkuu yeyote katika nchi ya Rombo wakati huo,ila kulikuwa na watu wachache wachache mno walioongozwa na wakubwa wao,kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine za kilimanjaro kabla ya kusimamishwa wakuu. Katika nchi ya useri tu kulikuwa na mkuu,lakini useri haikuwa sehemu ya milki ya mamba,mtu mmoja jina lake moosinyi wa ukoo wa kumba alikuja na wafuasi wake wakakaa keni,na kijukuu chake jina lake ukongi alipigana na marawite wa mamba kwa muda,ingawa alishindwa, hata hivi alifanywa mkubwa wa nchi ya chimbili chini ya marawite.chimbili ni nchi iliyokati ya mriti na mkuu.urio mwanae ukongi alimuari mafuluke,pia akashindwa baada ya vita vikali vya siku nyingi.katika vita hivi nchi iliachwa ukiwa wala haikuwa na ng'ombe,lakini mafuluke aliweka ng'ombe wake wengine kwa watu,na kwa miaka kadhaa walikaa kwa amani chini yake
urio alikuwa na wana wawili,mkubwa alikuwa Msangaro na mdogo aliitwa Horombo.
Msangaro alikuwa kijana mpole lakini horombo alikuwa mkali wala hawezi kutulia,akamwudhi sana baba yake kwa kuwaua ng'ombe waliowekwa kwao na watu wa mamba na kuila nyama yake,alikuwa na nguvu nyingi sana,tena mrefu kuliko watu wote wa nchi,hivyo hakuna aliyethubutu kumchokoza,katika ujana wake alijipatia sifa nyingi kwa sababu alimwua tembo peke yake,na watu wa waalenyi walipokuja kuchukua nyama ya tembo,aliwanyang'anya ng'ombe wao wote na kuwachinja kuwafanyia karamu watu,matendo aliyoyafanya yaliwaogofya sana watu wa keni mpaka walimwomba awe mkuu wao,maana waliona hakuna njia ila hii ya kupata amani katika nchi.
Lakini watu wa nchi zilizo jirani,yaani mriti,mengeve,chimbili, na mkuu hawakumkubali horombo,na kwa hivi alifanya vita nao akawanyanga'nya ng'ombe wengi sana.lakini ng'ombe wale aliowachukua kwa kweli walikuwa ng'ombe za watu wa mamba,