great chiefs in chagga tribe

in chagga language they are known as mangi
Those famous chiefs includes
mangi rongoma of kilema
mangi horombo of keni
mangi rengwa of machame
mangi mashina of mamba
mangi mosha of kirua
mangi marealle of marangu
mangi sina of kibosho
mangi rindi of moshi
mangi meli of moshi
mangi warsingi of uru
mangi ndeseruo of machame
mangi shangali of machame
mangi lokila of kibosho
mangi kikare of kirua
mangi kombo of kilema
mangi masaki of kilema

Thursday, July 29, 2010

Horombo

Hapo mwanzo wakuu wa mamba waliwashinda sana watu wa rombo kwa kuwa hapakuwa na mkuu yeyote katika nchi ya Rombo wakati huo,ila kulikuwa na watu wachache wachache mno walioongozwa na wakubwa wao,kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine za kilimanjaro kabla ya kusimamishwa wakuu. Katika nchi ya useri tu kulikuwa na mkuu,lakini useri haikuwa sehemu ya milki ya mamba,mtu mmoja jina lake moosinyi wa ukoo wa kumba alikuja na wafuasi wake wakakaa keni,na kijukuu chake jina lake ukongi alipigana na marawite wa mamba kwa muda,ingawa alishindwa, hata hivi alifanywa mkubwa wa nchi ya chimbili chini ya marawite.chimbili ni nchi iliyokati ya mriti na mkuu.urio mwanae ukongi alimuari mafuluke,pia akashindwa baada ya vita vikali vya siku nyingi.katika vita hivi nchi iliachwa ukiwa wala haikuwa na ng'ombe,lakini mafuluke aliweka ng'ombe wake wengine kwa watu,na kwa miaka kadhaa walikaa kwa amani chini yake
urio alikuwa na wana wawili,mkubwa alikuwa Msangaro na mdogo aliitwa Horombo.
Msangaro alikuwa kijana mpole lakini horombo alikuwa mkali wala hawezi kutulia,akamwudhi sana baba yake kwa kuwaua ng'ombe waliowekwa kwao na watu wa mamba na kuila nyama yake,alikuwa na nguvu nyingi sana,tena mrefu kuliko watu wote wa nchi,hivyo hakuna aliyethubutu kumchokoza,katika ujana wake alijipatia sifa nyingi kwa sababu alimwua tembo peke yake,na watu wa waalenyi walipokuja kuchukua nyama ya tembo,aliwanyang'anya ng'ombe wao wote na kuwachinja kuwafanyia karamu watu,matendo aliyoyafanya yaliwaogofya sana watu wa keni mpaka walimwomba awe mkuu wao,maana waliona hakuna njia ila hii ya kupata amani katika nchi.
Lakini watu wa nchi zilizo jirani,yaani mriti,mengeve,chimbili, na mkuu hawakumkubali horombo,na kwa hivi alifanya vita nao akawanyanga'nya ng'ombe wengi sana.lakini ng'ombe wale aliowachukua kwa kweli walikuwa ng'ombe za watu wa mamba,

Rombo

Kadiri ilivyojulikana,habari za zamani
rombo ni habari za jamaa nyingine ambazo hapana moja iliyokuwa ya maana sana.hapakuwa na mkuu katika nchi ya rombo mpaka wakati wa HOROMBO,na hata hivyo haikudumu sana baada ya kufa horombo isipokuwa katika useri.
Sababu ya tofauti kubwa ya warombo na wachaga wengine si vigumu kuieleza,nchi ya rombo ni nzuri kwa mifugo ya ng'ombe,lakini sehemu nyingine ya kilimanjaro inayokaa watu ni nchi ya kilimo hasa.wachaga hasa walikuwa walimaji,lakini warombo walipenda kufuga ng'ombe
na sababu ya tofauti ni hizi
1.kwa desturi watu wafugao ng'ombe hawashirikiani sana pamoja
wanapenda zaidi kukaa kila jamaa peke yake,hivyo warombo walishika desturi zao za zamani walizozipata kutoka ukamba ambako hapakuwa na wakuu wa kutawala
2.wale waliokuwa walimaji walitamani sana kupata ng'ombe ,hivyo walikuwa tayari kujiweka chini ya mkuu awezaye kupigana na jirani na kukamata ng'ombe zao hivyo kuwatajirisha kwa mifugo
3.mifereji ya maji kwa walimaji haikuwezwa kutengenezwa na kuangaliwa bila watu kushirikiana pamoja chini ya wakuu waliojulikana au kuchaguliwa. Lakini nchi ya Rombo ni kavu,wala haina vijito vilivyo lazima kutumika katika mashamba.basi hapo warombo walikuwa hawana haja ya kujiweka chini ya watawala,ndiyo sababu wakuu hawakuwekwa katika nchi yao.

Rongoma

katika habari za kilema tulifika mpaka wakati wa kombo alipourithi utawala toka kwa Nyange.katika utawala wake,kilema iliingiliwa na Ngaramite mkuu wa marangu aliyesaidiwa na watu wa chimbili na wengine wa ugweno.Kombo alikimbia pamoja na watu wake wote mpaka Kirua alipotawala MOSHA.Basi ikatokea ya kuwa Mosha alimtamani mkewe Kombo akajaribu kumshawishi ampe sumu mumewe na mwanawe RONGOMA pia.lakini yule mwanamke alikimbia akarudi kilema,na Kombo na watu wote walimfuata.mara alipopata habari hii,ngaramite aliingia tena kilema pamoja na rafiki zake wagweno.kombo alitaka kukimbia tena,lakini mke wake alijipatia silaha akawaongoza watu wa kilema kupambana na adui,na hapo Kombo akaona aibu,na yeye mwenyewe akaja akawaongoza.nao watu wa kilema walijipa moyo kwa kuona ushujaa wa yule mwanamke,wakapigana kwa nguvu nyingi sana wakawashinda adui zao.
Baada ya hayo Kombo alinuia kumpiga Mosha kwa kufanya lile tendo ovu wakati alipokuwa mgeni wake.akampeleka mwanawe Rongoma utaita ili apate msaada lakini alikawia sana,na huku nyuma yeye mwenyewe alipata msaada kutoka ugweno akawashinda watu wa Mosha,akawaweka chini yake,baada ya muda kupita Rongoma alirudi kutoka utaita akileta watu wa kupigana pamoja nae,na kwa kuwa nchi ya kirua ilikwisha wekwa chini ya baba yake,walifanya vita na marangu iliyotawaliwa na masanjuo,wakateka sehemu ya nchi ile.
Baada ya miaka michache kupita kombo alijiuzulu na mwanawe RONGOMA Akaushika utawala.wakati huo huo kilewo aliyekuwa mtawala wa marangu akafa pia,mara ile Rongoma alipeleka tarishi kuwakaribisha wanawe kilewo waje kukaa nae ili apate kuwatunza,maana kwa kuwa ni mzao wa mremi alifanya kama anataka kuwa kaka yao,silawe na ishosho wana wawili wa kilewo walikwenda kilema wakapokewa vizuri,lakini walipotaka kurudi kwao,Rongoma aliwafanya wafungwa,kisha aliingia marangu na kujitangaza mkuu kwa haki,kwa kuwa ni mkubwa wa ukoo, uliotoka wakuu wa nchi zote mbili.

Kilema

watu waliokuja kukaa katika nchi ya kilema walitoka zaidi utaita,upare na ukamba; na kama zilivyokua pande nyngne hawakuanganika,ila walitawanyika wakakaa kila jamaa na mkuu wake,mpaka ngowi alipotoka marangu
huko kilema alifanya urafiki na moye mjukuu wa kinyaga aliyeuawa kwa amri ya lyimo,moye alimshauri ngowi achinje ng'ombe duwe 100 aliowapata kwa riwa wa marangu mwanawe na kuwafanyia karamu watu wa koo za kilema,kwa njia hii alijifanya apendwe na watu,na kwa kuwa waliyakumbuka yale yaliyowapata watu wa marangu walikuwa wamekwishajua faida ya kuwa na mkuu hivyo wakamchagua mremi mwana wa ngowi awe mkuu wao,
hivyo basi wakuu wa marangu na wale wa kilema ni wa ukoo mmoja.

Wakuu wote ila MOSHA aliyetawala sehemu ya juu ya kilema walimtii mremi na hata yeye alitiishwa baadaye akawa chini ya mremi.mremi alipokua mzee alimwachia ngowi mwanae ukuu.katika siku za ngowi paliondokea watu wengine waliokuja kukaa sango bondeni mwa mlima,na mkubwa wao ni kitangu,wageni hawa walikuwa watu wa vta kweli kweli,wakijilinda sana wasiingiliwe na ngowi,naye hakuweza kuwashinda,maana hakutawala siku nyingi akafa kabla ya mremi baba yake.
Iko hadithi ya kuwa ngowi alikufa kwa kuwa alitoa siri ya kutokewa na Mungu na kuamriwa kutawala kwa hekima na haki,alirithiwa utawala na nyange mwanawe,lakini hakuwa na nguvu wala uwezo wa kutawala,kabla siku nyingi kupita musuo mjomba wake alimwondoa katika utawala,lakini nyange alikimbilia mamba na kwa msaada wa soka mwanawe moye aliekuwa rafiki wa ngowi wa kwanza,alimwomba mafuluke mkuu wa mamba aje kumsaidia kumfukuza musuo,naye musuo alishindwa upesi sana akauawa vitani,sasa nyange akaurudia utawala,akatawala mpaka uzeeni,kisha akaiacha kazi ya utawala na Kombo mwanawe akaurithi utawala mahali pake.

strike at st.joseph

Ni kama miez miwil imepita toka mgomo huo ulipotokea baada ya uongoz wa chuo kutangaza ongezeko la ada na wanafunz kugoma kuendelea na vipind ili kushinikiza kutolipa ongezeko hilo pamoja na maelezo ya kina toka kwa principal.hali hiyo ilipelekea kusimamishwa masomo kwa wanafunz wote wa mwaka wa kwanza kwa muda usiojulikana na pia wanafunz wengine kumi na nne kusimamishwa!

Friday, February 19, 2010

Korongo la kishingonyi

Hilo ni korongo lilitonganisha kilimanjaro kakika pande mbili yaani mashariki na magharibi katika nchi ya uchagga korongo hili linakumbukwa hasa kwa mambo yafuatayo
1.hapa ndipo watoto walipozikwa hai ili kufunga mapatano waliyofanya horombo na rongoma.
2.mpaka unaotenga nchi za rombo na vunjo
3.ilipoanzia milki ya rongoma mpaka nchi iitwayo nanga.
those who wish to follow me i welcome with all my hands

kilema hospital

those who wish to follow me i welcome with all my hands

Wednesday, February 17, 2010

condomising and the society

condomisimg means that using of condoms
We do say that people should use condoms so that to reduce new infections of hiv/aids.
It's obvious that use of condoms has led into increase in rate of doing sex! also you have to believe that it increases unsafe sex and new infections!

kilema

welcome to kilema!
Observe it's peculiarity and much more! Just ask n you will be answered promptly!

st.joseph college of engineering and technoly

a college operated by dmi-sisters in dar es salaam,luguruni area
the college offers various bachelor degrees in
+civil eng
+electrical and electronics eng
+electronics and communication
+computer engg
+information system and networking
also in the academic year 10/11 there will be 2 more courses!
+aeronautic engg
+mechanical engg